Mwandishi Wetu ,Dodoma
CHANZO cha kuwapo mauzo ya kangomba kwenye zao la korosho kimetajwa kuwa ni kutokana na gharama kubwa za kuandaa mashamba, kupalilia pamoja na bei kubwa za viuatilifu.
Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Christine Ishengoma amesema bungeni leo, Mei 17 kuwa kuna gharama kubwa ambazo wakulima wa kawaida hawawezi kuzimudu hivyo kuingia mikataba ya kupata fedha zitakazosaidia kuhudumia mashamba yao
“Hali hii inatokana na wakulima kukosa usaidizi wa Serikali wakati wa kuandaa msimu mpya wa mazao.”amesema Dk Ishengoma