25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Kilwa walilia elimu bora

FLORENCE SANAWA-KILWA

Wakazi wa kitongoji cha Mbate kata ya Kikore wilayani Kilwa Mkoani Lindi wameiomba serikali kuwajengea shule itakayohamasisha elimu kutokana na watoto wengi kuacha shule kwa kuhofia kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 21 pamoja na mazingira wanayopita kutokuwa salama hasa kwa watoto wa kike ambao wako Katika hatari zaidi.

Akizungumza na MTANZANIA ilipotembelea kitongoji hicho mkazi wa eneo hilo Hassan Kikarango amesema kuwa watoto wa kitongoji hicho wanashindwa kuanza shule wakiwa na umri wa miaka saba na badala yake wanaanza wakiwa na umri mkubwa hali ambayo huwakatisha tamaa mapema na kupelekea wengine kupata ujauzito ambao umekuwa ni kikwazo zaidi kwa watoto wakike

“Wakati mwingine njiani watoto wanakutana na wanyama wakali wakiwemo simba, tembo na wakati mwingine wananyeshewa na mvua, hivi mtoto anawezaje kutembea mwaka mzima Katika eneo ambalo ni hatarishi kwake na akafanikiwa ni wachache sana waliofanikiwa kufika darasa la saba hivyo tunaiomba serikali ituangalie kwa jicho la huruma”

Kwa upande wake Mratibu Mwandamizi wa mradi wa elimu bora unaoendeshwa na Madrasa Zanzibar na Shirika la Agakhan Foundation  Shaibu Mandova, amesema kuwa baada ya shirika hilo kuona adha wanayopata watoto wadogo walilazimika kujenga vituo shikizi 40 na kuweka walimu 80 lakini bado mahitaji ni makubwa zaidi na kwamba wamefakiwa kupata watoto zaidi ya 1000 wenye umri wa kuanzia Miaka 5 hadi 9 Huku baadhi yao wakifanikiwa kujiunga na elimu ya msingi ambayo hulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles