25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri aeleza miradi ya maji ‘inavyopigwa’

Na ARODIA PETER

-DODOMA

WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, amesema kumekuwa na changamoto ya usimamizi wa miradi ya maji nchini, hususan kwenye gharama halisi za miradi.

Alisema kwamba, kulikuwa na mtandao mpana wa upigaji wa fedha za miradi ya maji kuanzia halmashauri, mkoani hadi wizarani.

Akihitimisha hotuba ya bajeti ya wizara yake bungeni jana, Profesa Mbarawa alisema miradi mingi iliyojengwa kati ya mwaka 2010 na  2015, ilijengwa chini ya kiwango tofauti na iliyoanza kujengwa mwaka 2016 hadi sasa.

“Kutokana na upungufu huo, watumishi 14 wameondolewa kwenye sekta hiyo ndani ya wiki mbili, ambao walikuwa ni vichochoro vya kupiga fedha za Serikali kwenye miradi ya maji, ambapo pia bodi yote ya mfuko wa maji imeondolewa.

“Wakati wa kupiga fedha za Serikali sasa umekwisha na haikubaliki, imetosha, asiyeweza kulinda miradi hii, aondoke, hakuna cha mkurugenzi wala nani, maana lazima wizara inyooke,” alisisitiza Profesa Mbarawa.

Katika hoja hiyo, Profesa Mbarawa alisema kwa sasa wizara inatarajia kuwa na mpango mkakati wa kujua gharama za miradi na bei halisi ambapo watendaji watapata thamani ya fedha inayowekezwa kwenye miradi na ndiyo itakayotumika kwenye miradi yote chini ya Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA).

Kuhusu tozo ya wachimbaji visima vya maji kwa watumiaji binafsi wa nyumbani, Profesa Mbarawa alisema:

“Kuanzia leo, Serikali imefuta tozo za visima vya maji kwa watumiaji binafsi kwa matumizi binafsi ya nyumbani na Watanzania hawa, lazima wapate maji safi na salama, kwani hatutaki kuwaona wakilalamika au wanapata shida,” alisisitiza.

Profesa Mbarawa alisema eneo la tozo kwa watumiaji maji chini ya ardhi, yaani tozo ya uchimbaji visima lililalamikiwa sana na wabunge na wananchi kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles