27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ahadi hewa ya ndoa ni kosa la ubakaji India

DELHI, INDIA

MAHAKAMA ya Juu ya India imetoa uamuzi kuwa iwapo mwanaume atashindwa kutimiza ahadi ya kumuoa mwanamke huku akiwa ameshafanya naye tendo la ndoa, hilo litahesabiwa kosa la ubakaji.

Katika uamuzi muhimu, mahakama imepitisha uamuzi wa mahakama ya awali na kumtia hatiani daktari mmoja nchini humo kwa kosa la ubakaji.

Kwa mujibu ya waendesha mashtaka, tukio hilo lililotokea  katika Jimbo la Chhattisgarh, daktari huyo alikuwa na makubaliano ya uhusiano wa kingono na mlalamikaji baada ya kumuahidi kuwa atamuoa, lakini hakutimiza ahadi hiyo badala yake akaenda kumuoa mwanamke mwingine.

Majaji L Nageswara Rao na MR Shah walisema mwanamke alimruhusu daktari kufanya ngono naye akiamini alikuwa ana lengo la kumuoa, hivyo hilo haliwezi kuchukuliwa kuwa alimruhusu kufanya tendo la ngono kwa hiari.

Majaji walisema mshtakiwa alikuwa na lengo la wazi  la kutomuoa, na kuongeza kuwa tendo la ngono linalofanyika bila dhana halisi haliwezi kuchukuliwa kuwa hiari.

Hata hivyo, mahakama ilipunguza kifungo cha miaka 10 alichokuwa amefungwa na Mahakama ya Mwanzo na kumpa adhabu ya kifungo cha miaka saba jela, ambacho majaji walisema ilikuwa cha lazima ili mshtakiwa akabiliwe na athari za uhalifu alioutekeleza.

Hii si kesi ya kwanza. Kwa mujibu wa data za Serikali za mwaka 2016, polisi walirekodi kesi 10,068 za aina hiyo za ubakaji zinazofahamika kama za ‘waathiriwa wa ahadi ya ndoa.’

Lakini pia majaji wa Mahakama ya Juu waliishauri mahakama za mwanzo kuchunguza kwa makini iwapo mwanamume aliahidi kumuoa mwathirika au kulikuwa na njama nyingine tangu mwanzo na kwamba alifanya tendo la ngono kwa lengo tu la kuridhisha nafsi yake.

Hii ina maana kuwa iwapo mwanaume atathibitisha kuwa kweli alitaka kumuoa mwanamke lakini akabadili nia hiyo baadae, bado haitakuwa ubakaji.

Aidha haichukuliwi kama ubakaji ikibainika kuwa mwanamke alikuwa na njama mbaya tangu mwanzoni mwa uhusiano.

Lakini kama kweli tendo hilo lilifanyika kwa lengo fulani si rahisi kuthibitisha ukweli wake, na uamuzi huachiwa majaji, hali ambayo imezua hofu kuwa sheria hiyo inaweza kutumiwa vibaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles