27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Trump kulitangaza ‘Udugu wa Kiislamu’ kundi la kigaidi

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump wa Marekani anapanga kulitangaza Udugu wa Kiislamu kuwa la kigaidi, hatua ambayo inaweza kulisababishia kundi hilo kongwe zaidi la Kiislamu nchini Misri kuwekewa vikwazo.

Msemaji wa Ikulu ya White House mjini hapa, Sarah Sanders, ametoa taarifa kwa njia ya barua pepe, akieleza Trump ameijadili hatua hiyo na washauri wake wa kiusalama pamoja na viongozi wa kikanda wenye mtazamo sawa na wake kuhusu kundi hilo.

Ripoti ya gazeti la New York Times la hapa, ambayo imethibitishwa na ofisa mwandamizi wa Serikali ya Marekani, imesema Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri alimuomba Trump kuchukua hatua hiyo wakati alipofanya ziara nchini hapa Aprili 9 mwaka huu.

Licha ya wasiwasi ulioelezwa na wabunge wa vyama vyote nchini Marekani kuhusu rekodi mbaya ya haki za binadamu ya Rais al-Sisi, Trump alimsifu kiongozi huyo, akimwita ‘rais bora kabisa’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles