30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Grace Products yatoa msaada kwa Albino Dar

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Kampuni ya Grace Products Limited imetoa msaada wa mafuta ya kupaka na sabuni maalum kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ili viwasaidie katika utunzaji wa ngozi na nywele zao.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huo leo Aprili 25, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo  Dk Elizabeth Kilili amesema bidhaa walizotoa zimetengenezwa maalum kwa albino ili kuwakinga na magonjwa ya ngozi lakini pia kulainisha nywele zao.

Dk. Elizabeth amesema watu wenye ualbino wanahitaji msaada wa hali na mali lakini pia kuonyeshwa upendo kwani kuna muda huwa wanajihisi ni watu wasio na thamani katika jamii lakini pia amewataka Watanzania kuacha kuwanyanyapaa Albino.

“Hii si mara yangu ya kwanza kutoa bidhaa hizi kwa watu wenye ualbino na ambao wamewahi kutumia wamerudisha majibu kuwa ni nzuri na zinawasadia katika ngozi na nywele hasa kwa kina mama ambao mwanzoni walikuwa wanashindwa hata kusuka kwasababu ya nywele zao kuwa ngumu na kujifunga,” amesema.

Naye Mbunge wa Temeke (CCM), Abdallah Mtolea amewataka Watanzania  kuisaidia jamii yenye uhitaji kwa kile kidogo wanachokipata kama alivyofanya Dk. Elizabeth na kila mtu anaweza kufanya hivyo na sio kila kitu lazima Serikali ifanye.

“Zamani tulikuwa tunaagiza nje ya nchi mafuta ya kupaka na sabuni kwa ajili ya watu wenye ualbino ili kutunza ngozi zao, Grace amefikiria nje ya kupata faida lakini ametengeneza bidhaa ambazo zitawasaidia na wenyewe wamekiri kuwa zinawasaidia hivyo ameona kupata faida ni kuisaidia jamii inayomzunguka pia,” amesema Mtolea.

Kwa Upande wake Katibu wa Chama cha  watu wenye ualbino Tanzania (TAS), Gaston Mcheka amesema kuanzia sasa Dk Elizabeth, Mbunge Mtolea na Msanii Banana Zorro wameteuliwa kuwa wanachama wao kwa nafasi ya wanachama wa heshima wanayopewa wadau na watu wenye mapenzi mema na chama hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles