25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Mwinyi Zahera apiga mkwara mzito wachezaji Yanga

Lulu Ringo, Dar Es Salaam

Kocha mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amesema mchezaji yeyote ambaye hatotokea katika mazoezi ya kesho Aprili 26 kwa madai ya kudai mshahara hatomjumuisha katika kikosi chake hadi mwisho wa msimu wa ligi 2018/19.

Zahera amesema wachezaji wawili tu Kelvini Yondani na Papy Tshishimbi ndiyo wachezaji pekee wenye ruhusa

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Alhamisi Aprili 25, kocha huyo amesema ameshangazwa na maswali mengi kutoka kwa waandishi wa habari juu ya kugoma kwa wachezaji hao kwani hakuwa na taarifa yoyote.

“Wachezaji hawa sidhani kama watapata mtu kama mimi maisha yao yote, ninawasaidia mambo mengi nje na ndani ya mpira hata mambo ya maisha yao.

“Kabla ya kufanya hili walilofanya leo nafikiri wangejiuliza mara mbili juu ya uamuzi waliochukua kugoma kufanya mazoezi tena bila kunipa taarifa,” amesema Zahera.

Kutokana na tetesi hizo za wachezaji hao kugoma, Mwinyi Zahera amemtaka Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Salehe, kutomjumuisha kwenye kikosi chake cha msimu huu mchezaji yeyote atakayegoma kufika mazoezini kesho.

“Nimemwambia Hafidhi awaambie wachezaji wote atakaye kosa mazoezi ya kesho hatokuwa mmoja wa wachezaji wa kikosi changu hadi mwisho wa msimu huu.

“Kwanini wameamua kudai mshahara mwezi moja kabla ya ligi kumalizika na wanajuwa ni wakati gani walipata mishahara yao ya mwisho tena waulizeni ni wakati gani walipata mishahara yao ya mwisho,” amesema Zahera.

Katika hatua nyingine Kocha huyo amesema iwapo msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amepanga kwenda kumshtaki kutokana na tetesi za kumfukuza Meneja wa Timu ya Yanga, Narid Haroub ‘Cannavaro’ akamshtaki kama anaona anaijua sheria kuliko watu wengine.

“Manara amezoea kuongea maneno mengi sana yasiyo na maana, kama anasema atanishitaki kwa mambo ya ‘Cannavaro’ aende akanishitaki kama kumshitaki mtu ni mpaka uandike au useme kwenye mitandao ya kijamii, kama anadhani yeye anajua sheria kuliko watu wote duniani. anajidanganya,” ameeleza Kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,430FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles