22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Man City wapata pigo kwa De Bruyne

MANCHESTER, ENGLAND

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester City, wanaweza kumkosa kiungo wao mahiri, Kevin De Bruyne, hadi mwishoni mwa msimu kutokana na kuumia nyama za paja mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mchezaji huyo aliumia katika mchezo dhidi ya Tottenham na kutolewa nje huku nafasi yake ikichukuliwa na Fernandinho, lakini mchezo huo ulimalizika kwa Manchester City kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kutokana na tatizo hilo, De Bruyne anaweza kuwa nje ya uwanja na kuikosa michezo mitatu ya Ligi Kuu iliyosalia kabla ya kumalizika kwa msimu huu. Michezo hiyo ni Burnley ambao watakuwa nyumbani Aprili 28, huku Mei 6, mwaka huu Man City wakiwa nyumbani kucheza dhidi ya Leicester City na Mei 12 wakiwa ugenini kupambana na Brighton.

Hata hivyo, mchezaji huyo anapambana kuhakikisha anakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa fainali wa Kombe la FA mwezi ujao dhidi ya Watford kwenye Uwanja wa Wembley.

Mchezaji huyo amekuwa nje ya uwanja mara kwa mara msimu huu kutokana na kusumbuliwa na majeraha. Mzunguko wa kwanza wa ligi kabla ya Oktoba mwaka jana mchezaji huyo alicheza mchezo mmoja tu kutokana na kusumbuliwa na tatizo la goti.

Mapema Machi mwaka huu, mchezaji huyo aliumia nyama za paja na kumfanya awe nje ya uwanja kwa mwezi mmoja na sasa ameumia tena ambapo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili hadi tatu.

Kukaa kwake nje ya uwanja kulimfanya ampe nafasi kinda wa timu hiyo, Phil Foden, kuonesha ubora wake ndani ya kikosi cha kwanza. Foden alifunga bao lake la kwanza katika mchezo dhidi ya Tottenham ikiwa ni siku nne tangu Man City walivyofungashiwa virago na wapinzani hao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles