33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Brela yatahadharisha wanasheria kudanganya wafanyabiashara

Na DERICK MILTON

-BARIADI

WAKALA wa usajili wa biashara na leseni nchini (BRELA) umewataka wanasheria ambao wanawasaidia wafanyabishara kusajili biashara zao kutowadanganya na badala yake wafuate taratibu zote na kanuni zilizowekwa na mamlaka hiyo katika usajili wa bishara.

Mamlaka hiyo imesema kuwa licha ya wanasheria kutambuliwa kama watu sahihi kuwasaidia wafanyabishara kusajili biashara zao, wanatakiwa kufuata kanuni na taratibu zote zilizowekwa.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa utawala Blera Bakari Mketo,  wakati akizungumza na wafanyabishara wa mji wa Bariadi Mkoani Simiyu  wiki hii ambao tayari wamesajili biashara zao kwa kutumia mfumo mpya wa usajili kwa njia ya mtandao.

Mketo alisema wamekutana na baadhi ya wafanyabishara kutoka Simiyu, ambao waliambiwa na wanasheria kuwa baadhi ya vitu havihitajiki wakati wa kusajili jambo ambalo siyo kweli.

“ Mmoja wa wafanyabishara kutoka hapa Simiyu aliambiwa na mwanasheria kuwa baadhi ya nyaraka hazitakiwi, lakini huyu mwenye biashara akatupigia simu tukamwambia siyo kweli nyaraka zote zinahitajika na akafanikiwa kusajili,” alisema Mketo.

“ Tuwaombe wanasheria, najua tunafanya kazi kwa pamoja wanatakiwa kufuata sheria na taratibu zote zilizowekwa na Brela katika kuhakikisha wanawasaidia wafanyabishara wanasajili biashara zao vizuri,” alisema Mketo.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Brela imefanikiwa kuongeza idadi ya wafanyabishara ambao wamesajili biashara zao, ambapo kwa kipindi cha robo ya tatu iliyoisha machi 31, 2019 wamesajili makampuni 4678 sawa na asilimia 69.

Elizabeth Samweli ni mmiliki wa kampuni ya Mlashi General Supplies iliyoko Bariadi, ambaye baadhi ya nyaraka za mkataba wa makubaliano  na Brela ziliondolewa na mwanasheria wake wakati akiziandaa.

Samweli alieleza kuwa baada ya kuondolewa kwa nyaraka hizo waliamua kupiga simu Brela kuulizia  kama ni sahihi nyaraka hizo kuondolewa, ambapo waliambiwa siyo kweli zinatakiwa kuwepo na kufanikiwa kusajili biashara zao.

Kwa upande wake, Afisa kutoka Brela, Suzan Senso alisema kupitia mfumo mpya wa usajili kwa mtandao (online Registration System), watu wengi wameanza kuuelewa na kuanza kusajili biashara zao kwa kasi.

Aliwataka wafanyabishara nchini kuendeea kusajili kwa kutumia mfumo huo, ili kuondoa usumbufu na gharama za kusajili kwenda Dar es salaam,  na zaidi akiwataka kupiga simu Brela kwa ajili ya kupata ufafanuzi wowote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles