29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Jumuiya ya wazazi yaonya wanaotumikisha watoto

Na ALLAN VICENT- TABORA

JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Tabora, imewataka wazazi na walezi wanaotumikisha watoto kazi ngumu au hatarishi kuacha mara moja kabla hatua hazijachukuliwa.

Onyo hilo limetolewa hivi karibuni na Meya Mstaafu na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Gulam Dewji, katika sherehe za maadhimisho ya wiki ya wazazi zilizofanyika katika Kata ya Kigwa wilayani Uyui.

Aliwataka wazazi na walezi wote kukaa na watoto wao vizuri kwa kuhakikisha wanawapa elimu, malezi bora na kuwafundisha maadili mema na si kuwanyanyasa kwa kuwatumikisha katika ajira hatarishi.

Aliwakumbusha kuwa watoto wadogo ni hazina kwa taifa na ndio viongozi wa kesho wa chama na Serikali, hivyo wanapaswa kulelewa katika misingi na maadili mema ikiwemo kulindwa ili wasipotoke kimaadili.

Aliwataka watendaji wa mitaa na vijiji kuhakikisha haki za watoto zinalindwa na kukemea vitendo vya uonevu au unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya wazazi au walezi.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Uyui, Lubasha Makoba, alisema jukumu la Jumuiya ya Wazazi ni kuhakikisha kila mzazi anawapa elimu na malezi bora watoto wake ili kuepuka mporomoko wa maadili.

Aidha, aliwataka wazazi kuwa mfano mzuri wa kuigwa na watoto wao kwa kujiepusha na tabia zisizofaa ikiwemo kutongoza wasichana wadogo au wanawake kuwataka kimapenzi wavulana wadogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,905FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles