29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

RC ataka kilimo cha kahawa kiongezwe maradufu

NA TIMOTHY ITEMBE  

MKUU  wa Mkoa wa Mara,  Adam  Malima amezitaka halmashauri   zinazojishugulisha na kilimo cha    kahawa kuhakikisha kilimo hicho kinapanda kutoka tani 2000 hadi tani 3200 kwa mwaka ifikapo mwaka 2022.

Malima alisema mkakati mwingine wa mkoa huo katika   kahawa ni kuhakikisha   Mara inalima kahawa kwa wingi na  yenye ubora ili kuwavutia wanunuzi na kuongeza kipato.

“Tunahitaji kilimo cha kisasa chenye tija   kuongeza wingi na ubora  wa kahawa.

“Kwa hali hiyo tunatarajia kuwa na soko la kahawa hapa hapa Tarime badala ya kusumbuka kwenda kutafuta masoko nje ya Tarime.

“…Tutakuwa tumepunguza gharama za usafirishaji ambazo zinatutesa huku tukipata fedha kidogo ya kuendeshea shughuli za maendeleo ikiwamo ya  familia,”alisema Malima.

Alizitaka halimashauri za  Tarime, Butiama, Bunda, Serengeti na Rorya   kuandika andiko la kuomba mkopo wa fedha ifikapo Aprili 30  kutoka benki   ili kuongeza jitihada za kilimo cha kahawa   ndani ya miaka mitano.

Mmoja wa wajumbe wa Bodi ya kahawa, Melkiad Masawe alisema   kazi ya bodi ni kutafuta masoko.

Alisema ili  wakulima waweze kunufaika na kilimo cha kahawa ni sharti walime kwa kuzingatia kanuni za kilimo   na   kujiandikisha katika daftari la kilimo hai.

Kikao hicho cha wadau wa    wakahawa   kilifanyika Nyamwaga wilayani Tarime   kujadili mkakati wa kufikia lengo la tani 5000 ifikapo mwaka 2022.

Ofisa kilimo na Umwagiliaji Wilaya Tarime,Sluvanus Gwiboha alisema  kuhakikisha kuwa lengo linafikiwa sharti wakulima wapande kahawa ya vikonyo.

Mkakati uliopo kwa halmashauri ya Tarime ni kulima kahawa kwa njia ya vikonyo na mbegu ili kuongeza uzalishaji kwa eneo kutoka tani 0.8 hadi tani 1.5 kwa hektaa.

Mwingine ni kuongeza kilimo cha  kahawa kutoka tani 2000 hadi tani 3200 kwa mwaka na kuandaa vitalu vitatu vitakavyozalisha miche 1,005,000 ifikapo 2021/2022.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles