NA MOHAMED MHARIZO
MATUMAINI ya timu ya soka ya vijana ya Angola kutinga nusu fainali ya michuano ya Afrika (Total U-17 Africa Cup of Nations) na kufuzu fainali za Kombe la Dunia yamebaki kwa Tanzania (Serengeti Boys).
Angola ina pointi tatu kwenye kundi A, baada ya kuifunga Uganda bao 1-0, kwenye mchezo wa kwanza, inaamini kuwa itaifunga Tanzania na kuungana na Nigeria kutoka kundi hilo kufuzu fainali za Kombe la Dunia.
Kocha Mkuu wa Angola, Pedro Soares, alisema bado wapo kwenye mbio za kufuzu Kombe la Dunia zitakazofanyika baadaye mwaka huu nchini Brazil.
“Tulipambana ili tuifunge Uganda lakini tulishindwa, walituzidi kimbinu lakini hatuwezi kukata tamaa, tutapambana tushinde mchezo ujao dhidi ya Tanzania.”
Alisema wanauchukulia umuhimu mkubwa mchezo wao na Tanzania kesho Uwanja wa Taifa.
Tayari Nigeria imetinga nusu fainali ya michuano hiyo na pia kufuzu fainali za Kombe la Dunia.
Kila kundi kwenye michuano hiyo ya Afrika itatoa timu mbili zitakazofuzu fainali za Kombe la Dunia.