22.7 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Cameroon yatinga nusu fainali, yafuzu Brazil

NA MOHAMED MHARIZO

TIMU ya soka ya vijana ya Cameroon ya umri chini ya miaka 17, imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Afrika kwa umri huo, baada ya kuifunga Morocco mabao 2-1 katika mchezo  uliochezwa jana Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

 Mchezo huo wa kundi B ulioanza saa nane mchana, ulikuwa mkali huku kila timu ikitafuta ushindi.

Licha ya kutinga nusu fainali, ushindi dhidi ya Morocco umeifanya Cameroon kukata tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil baadaye mwaka huu. 

Morocco ambayo mchezo uliopita ilitoka sare ya bao 1-1 na Senegal, ilikuwa ya kwanza kufunga bao dakika ya 21 kupitia kwa Tawfik Bentayeb. 

Bao hilo liliizindua Cameroon ambayo ilijipanga vema na kuanza kuliandama lango na Morocco.

 Ili kuhakikisha inapunguza kasi ya mashambulizi ya Cameroon, Morocco ilifanya mabadiliko dakika ya 31, alitoka Jihad Moussalli na nafasi yake kuchukuliwa na Oussama Raoui.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika huku Morocco ikiwa mbele kwa mabao 1-0.

Kipindi cha pili, Cameroon ilicharuka na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa Morocco.

Dakika ya 60, Cameroon ilifanya mabadiliko, alitoka Nassourou Ben na kuingia Saad Bahir.

Mabadiliko hayo yaliisaidia Cameroon kwani dakika ya 72, ilifanikiwa kuisawazisha kupitia kwa Ismaila Seydou.

 Kuingia kwa bao hilo, kulizidisha hofu katika himaya ya Morocco iliyoamua kufanya mabadiliko dakika ya 80 ambayo alitoka Mohammed Essahel na kuingia Akram Nakach.

Mabadiliko hayo ya Morocco hayakuwa na faida zaidi ya hasara kwani dakika ya 89, Cameroon ilijipatia bao la pili na la ushindi  lililofungwa na Seidou, baada ya kumlamba chenga  kipa wa Morocco, Taha Amourid na kuuzamisha mpira wavuni.

Cameroon: Ricky Ngatchou, Daouda Amadou, Bere Benjamin, Gael Dibongue, Saidou Alioum, Leonell Wamba, Steve Mvoue, Nassourou Ben, Fabrice Ndzie, Manfred Ekoi, Patrice Ngolna.

Morocco: Taha Amourid, Jihad Moussalli, Anas Nanah, Oussama Targhalline, Mohammed Assahel, Bilal Ouacharaf, Tawfik Bentayeb, Achraz Ramzi, Yassine Ketcha, Faissal Boujemaoui na Saad Bahir.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,580FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles