Rais wa zamani wa Peru Alan GarcÃa, amefariki dunia baada ya kujipiga risasi kabla ya kukamatwa na polisi waliokuwa wamewasili nyumbani kwake kwa ajili ya kumkamata juu ya mashtaka ya rushwa.
Kifo cha GarcÃa kimethibitishwa na Rais wa sasa wa Peru, MartÃn Vizcarra.
Kabla ya tukio hilo, maofisa wa polisi walikuwa wametumwa kumkamata Garcia nyumbani kwake kwa madai hayo ya rushwa.
Kwa upande wa Waziri wa Mambo ya Ndani Carlos Morán aliwaambia waandishi wa habari kuwa polisi walipofika, GarcÃa aliomba kwenda kuoiga simu na kuingia ndani ya chumba na kujifungia kwa ndani.
Anasema dakika chache baadaye, walisikia mlio wa risasi ukitokea katika chumba alichokuwamo Garcia.
Polisi walilazimika kufungua mlango kwa nguvu na kumkuta GarcÃa ameketi kwenye akiwa na jeraha la risasi kwenye kichwa chake.
Katibu wa GarcÃa, Ricardo Pinedo, alisema rais huyo wa zamani alikuwa na silaha nne au tano nyumbani mwake, zawadi alizopata kutoka kwa wanajeshi, na kwamba alikuwa ametumia mojawapo ya hizo silaha kujiua mwenyewe.
Kupita mtandao wa Twitter, Rais Vizcarra amesema “alishtushwa” na kifo cha rais wa zamani na kutoa salam za pole kwa familia yake.
GarcÃa alishtakiwa kwa kuchukua rushwa kutoka kampuni ya ujenzi wa Brazil Odebrecht, shtaka ambalo awali aliwahi kulikana.
GarcÃa aliwahi kuwa rais wa tangu 1985 hadi 1990 na kuongoza tena kuanzia 2006 hadi 2011.