27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 200 kuchuana tafiti za kisayansi

TUNU NASSOR -DAR ES SALAAM

Wanafunzi wa Sekondari zaidi ya 200 wanatarajiwa kuchuana vikali katika maonesho ya kufanya Tafiti za kisayansi kwa wanasayansi chipukizi yatakayofanyika Julai 31 na Agosti mosi Mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 18, Mwanzilishi mwenza wa Taasisi ya Young scientist (YST), Gosbert Kamugisha amesema mpaka sasa wamepokea kazi za wanafunzi zaidi ya 600 ambazo watazichuja na kubaki 200.

“Kwa kushirikiana na wafadhili wetu ambao ni Karimjee Jivanjee Foundation(KJF) na Shell Tanzania tumefanikiwa  kutembelea shule mbalimbali na kuwaelekeza wanafunzi namna ya kufanya tafiti na ugunduzi wa teknolojia,” amesema Kamugisha.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Toyota Tanzania ambao ni wadhamini wa Karimjee Jivanjee Foundation, Yusuf Karimjee amesema taasisi hiyo itatoa ufadhili wa masomo ya Chuo Kikuu  kwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika maonesho hayo.

“Kuanzia Mwaka 2012 hadi mwaka jana KJF imekuwa ikitoa udhamini kwa wanafunzi wabunifu kupitia YST ambapo jumla ya wanafunzi 27  wamenufaika na ufadhili huo,” amesema Yusuf.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles