27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MOI yaita wenye mahitaji ya viungo saidizi

    Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

WATU wenye mahitaji ya viungo saidizi wameombwa kufika katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kupatiwa viungo hivyo bure.

MOI kwa kushirikiana kampuni ya BMVSS kutoka India wanatarajia kutoa bingo saidizi kwa wahitaji 600 watakaojitokeza.

Akizungumza na MTANZANIA mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Kitengo cha Vifaa Tiba Saidizi MOI , Dk Leah Mamseri,  alisema watu wenye mahitaji ya viungo hivyo waende kujiorodhesha hospitalini hapo.

“Taasisi ya BMVSS wanatarajiwa kufika na  kuanza kutoa vifaa saidizi kwa watu 600 Mei mwaka huu hivyo kwa sasa tunapokea wenye mahitaji kwa vipimo,” alisema Dk. Leah.

Alisema kwa wake wenye uhitaji wafike katika kitengo cha viungo saidizi kilichopo Moi ambapo watapatiwa maelekezo pamoja na vipimo.

“Huduma hii itatolewa bure na baada ya kambi hii itaendelea kutolewa kwa kuchangia gharama hivyo niwashauri wenye mahitaji kuchangamkia fursa hii kwani hakuna bima ambazo zina  fao linaloweza kulipia viungo hivi,” alisema Dk. Leah..

Kwa upande wake Ofisa Habari wa MOI, Patrick Mvungi alisema utoaji wa viungo ni mipango mkakati wa hospitali hiyo kuhakikisha inawafikishia huduma watanzania wenye kupata cha chini.

“Hii itakuwa fursa kwa watanzania ambao wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu kwa kukosa fedha za kupata viungo hivyo,” alisema Mvungi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles