Na MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
ANDIKO lenye fumbo alilolitoa mtandaoni Profesa wa sheria, Issa Shivji, kwamba anatafuta taasisi ambayo hajaitaja jina ili aipe tunu, limezua mjadala.
Mjadala huo unatokana na kulitoa andiko hilo katika wakati ambao kuna mnyukano wa hoja za kisheria kuhusu msimamo wa Bunge uliotolewa mapema wiki hii na kukaziwa na Spika Job Ndugai, kwamba hawako tayari kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad isipokuwa ofisi anayoiongoza.
Andiko hilo la mhadhiri huyo mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mbobevu wa sheria, ambalo aliliweka katika akaunti yake ya Twitter juzi na jana kusambazwa kwa kasi katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo whatsapp linasomeka hivi;-
“Wabobezi na wajuaji wazee wenye busara tele, vijana wenye usomi uliofurika mnisaidie namtafuta mtu maarufu aitwaye Taasisi. Yuko wapi, natamani kuonana naye, natamani kushika mkono wake, natamani nimbus, natamani nimkaribishe kwa chai, wazee wenye busara, vijana wenye madigrii mnisaidie.”
Shivji ambaye tangu uibuke mvutano wa hoja za kisheria kuhusu msimamo wa Bunge na CAG hajasikika akizungumza lolote kama mtaalamu, na hata alipotafutwa juzi na gazeti dada la hili la MTANZANIA Jumamosi, hakutaka kusema lolote.
Pamoja na hayo, tayari andiko lake hilo baadhi ya watu wametafsiri kwamba …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti lako la MTANZANIA