27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

JPM: Wakazi wa Ruvuma acheni kuvamia maeneo ya mapori

Anna Potinus – Dar Es Salaam

Rais Dk John Magufuli amewataka wakazi wa Ruvuma na watanzania kwa ujumla kulinda vyanzo vya maji na maliasili kwa kuacha kuvamia maeneo ya mapori kwa maendeleo ya nchi.

Dk Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi mkoani humo leo Aprili 6, katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa njia ya usafirishaji umeme ya Kilovolt 220 kutoka Makambako hadi Songea.

“Tuvilinde vyanzo vya maji lakini pia tusivamie maeneo ya misitu tusiwe wachokozi wa kwenda kuwachokoza tembo siku moja tutakuta hawapo, Sweden hakuna tembo na ndio maana tunataka waje huku waone wanavyojichunga wenyewe ili watupe fedha,” amesema.

“Kila mwaka hekta laki nne za miti zinakatwa na tusipowapelekea watu umeme hata hilo pori la Seluu halitapona na mimi siwezi kuwaagiza askari kuwazuia watu kwenda porini wakati hatujawapa umeme.,”

Aidha ameishukuru serikali ya Sweden kwa ushirikiano wao katika kufanikisha mradi huo uliosaidia kuokoa bilioni 9.8 ambazo zilikuwa zikitumika kuzalisha umeme wa mafuta.

“Mahitaji ya umeme katika nchi yetu ni makubwa na yataendelea kuwa makubwa kwa sababu tumeamua kuifanya kuwa ya viwanda kwa bahati mbaya bei ya umeme kwa uniti katika nchi yetu ni kubwa sana,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles