27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Dk. Nshalla apokea kijiti Fatma Karume TLS

Na ELIYA MBONEA

-ARUSHA

CHAMA cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), kimemchangua Dk. Rugemeleza Nshala kuwa rais mpya wa chama hicho kwa kura 647. 

Akitangaza matokeo hayo jana kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Bahame Nyanduga alisema jumla ya kura 1,227 zilipigwa.  

Alisema wagombea wa nafasi ya urais walikuwa; John Sekka aliyepata kura 29, Gasper Nicodemus kura 58, Godfrey Wasonga kura 123, Godwin Ngwilimi kura 354 na Dk. Rugemeleza Nshala kura 647. 

“Kwa niaba ya Kamati ya uchaguzi na mtangaza rasmi Dk. Nshala kuwa Rais mpya wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika TLS kwakupata kura 647,”alisema Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Nyanduga. 

Akizungumza mara baada ya kutangazwa Rais mpya wa TLS Dk. Nshala alisema ataendelea kupigania utawala wa sheria na kutekeleza matakwa ya TLS.

Alisema mbali ya kupigania utawala pia TLS itaendelea kuhakikisha wanachama wake wanapata mafunzo mazuri ya sheria.

“Tutahakikisha tunaendeleza wanachama wetu kupata elimu na kufanya kazi zao bila matatizo.

“Mawakili au Wanasheria wafanye kazi zao kwa uhuru bila kunyanyaswa, kutishwa na kuwekwa ndani ambako kumejitokeza hivi sasa. 

“Mawakili ni watu muhimu katika kuhakikisha nchi inatawaliwa chini ya utawala wa sheria kama Katiba inavyosema,” alisema Dk. Nshala. 

Kwa upande wake Rais wa TLS aliyemaliza muda wake Fatma Karume, alipongeza kuchaguliwa kwa Dk. Nshala akisema hana wasiwasi na uongozi wake kwani nichaguo la wanachama. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles