24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

MAANDAMANO YATOKEA MPAKA WA KENYA NA TANZANIA

Maandamano yametokea katika mji wa Namanga uliopo kati ya nchi ya Kenya na Tanzania.

Kwa mujibu wa Maofisa wa polisi maandamano hayo yalizuka baada ya kutekwa nyara kwa mfanyabishara mmoja wa Kenya ambaye waandamanji hao wanasema alipelekwa nchini Tanzania.

Waandamanaji hao waliojawa na ghadhabu walifunga barabara inayoelekea Tanzania na hivyo  kukatiza shughuli zote za uchukuzi.

Kwa mujibu mtu mmoja aliyekuwepo kwenye tukio, anasema hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi wakati maafisa wa polisi wa Tanzania walipowasili karibu na ukuta unaogawanya Kenya na Tanzania ambapo waandamanaji waliingiwa na mori na kuanza kukabiliana na maofisa hao ambapo walirusha mabomu ya machozi .

Wakati hali hiyo iliposhindwa kudhibitika , wanasema, maafisa wa polisi walipiga risasi hewani kwa lengo la kuwatawanya waandamanaji hao kutoka Kenya.

Maofisa wa Polisi wa Kenya wamekuwa wakipiga doria katika eneo hilo huku wakiwaomba waandamanaji hao kuwa watulivu.

Pamoja na mambo mengine, mfanyabiashara huyo anayejulikana kwa jina Moha alidaiwa kuchukuliwa kutoka eneo analofanyia kazi na gari lenye namba za usajili za Tanzania.

”Tangu alipochukuliwa usiku uliopita hajaonekana”, alisema mmoja wa wakaazi wa eneo hilo Odinga Nguduu.

Akizungumzia kuhusu ufungaji wa barabara mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe alisema kuwa ni makosa kwa kundi lolote kusimamisha magari yanayovuka mpaka.

Mwaisumbe alisema ni kinyume na sheria kufanya hivyo na kuwa watalazimika kutumia uwezo wa Serikali kusitisha ghasia hiyo pia aliwashauri wakaazi wa Namanga kuwa watulivu huku Serikali ikichunguza swala hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles