25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Tanesco kuongeza megawati 125

mtanzania kila siku grace kenethd.inddNA AZIZA MASOUD, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), linaendelea kupunguza makali ya mgawo wa umeme, baada ya kutangaza kuongeza megawati 125 ili kuhakikisha huduma hiyo inarudi katika hali ya kawaida.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba, alisema ili kuhakikisha nchi inarudi katika hali ya kawaida, mitambo hiyo itawashwa kwa awamu ndani ya wiki hii ambapo juzi wameanza kuwasha mtambo wa megawati 35 kutoka mtambo wa Symbion.

“Jana (juzi) mchana tuliwasha mtambo wa megawati 35 unaomlikiwa na Symbion, na kuongeza kiwango cha umeme katika gridi ya taifa na kupunguza tatizo la kukatika baadhi ya maeneo,” alisema Mramba.

Alisema megawati 90 zilizobaki zitawashwa wiki hii, ambapo mtambo wa Kinyerezi unatarajia kutoa megawati 70, wakati mtambo wa Symbion utatoa megawati nyingine 20.

Mramba alisema kupatikana kwa umeme huo, kutaendelea kuboresha huduma ya nishati hiyo, hasa mikoa ya Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma.

Alisema mahitaji ya umeme wakati wa mchana nchi nzima kwa siku moja, ni megawati 870 na usiku megawati 940, wakati umeme unaozalishwa ni megawati 720.

“Hali ya umeme itaendelea kuwa bora baada ya kuwashwa mitambo yote ya Kinyerezi kutokana na kuwapo hali mbaya katika mabwawa yetu,” alisema Mramba.

Alisema umeme unaozalishwa kwa maji, umepungua kwa asilimia 81.3 na kusababisha uhaba wa nishati hiyo.
Mramba alisema kuwashwa mitambo ya gesi, kumesaidia kupunguza makali ya mgawo.

Alisema kukatika umeme mara kwa mara kunasababisha shirika kupata hasara ya Sh milioni 50 kwa siku,

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles