23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kibanda: Ole wao wanaochafua magazeti ya MTANZANIA, RAI

Absalom Kibanda (from Kibanda)croppedNA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya New Habari (2006) Ltd inayochapisha magazeti ya MTANZANIA, RAI, Bingwa Dimba na The African, imelaani vikali, uzushi, uongo na upotoshaji wa hali ya juu unaofanywa na watu wasio na nia njema na kampuni
hiyo.

Jana watu hao wasio na nia njema na kampuni hiyo, hasa magazeti ya MTANZANIA na RAI, walitengeneza mfano wa magazeti hayo kisha kuyaweka kwenye mitandao ya kijamii, yakiwa na taarifa mbalimbali za uongo na uzushi.

Akizungumzia hali hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alisema ameshtushwa na hatua hiyo, lakini ni vema wasomaji na wafuatiliaji wa magazeti ya MTANZANIA na RAI, wakapuuza magazeti yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, kwani watu wanaofanya hivyo wamelenga kuyachafua kwa masilahi yao binafsi.

Kibanda alisema watu hao wenye nia ovu na magazeti hayo, juzi walitengeneza mfano wa gazeti la RAI likiwa na kichwa cha habari kisemacho “Gwajima: Nina imani na Lowassa katika kutimiza ndoto zangu” na jana wametengeneza MTANZANIA na kulisambaza kwenye mitandao ya kijamii likiwa na kichwa habari “Lowassa,
Kagame wahusishwa kifo cha Mch. Mtikila”.

“Tumeshtushwa na hatua hii ya kurudia uovu wao, tulipoona kwa mara ya kwanza wametengeneza gazeti feki la RAI ambalo lina sura inayofanana na gazeti letu halisi na kuliweka kwenye mtandao ili kuwaaminisha watu kuwa
gazeti linaloenda sokoni ndiyo lile ambalo lilikuwa na habari ambazo ni potofu, zenye mwelekeo wa uchochezi, tulipuuza. Hata hivyo, wahusika wa uovu ule wa awali tuliwabaini.

“Watu hawa wamerudia tena, sasa niseme inatosha, napenda kuwaambia wasomaji wa gazeti la MTANZANIA ambalo huchapishwa kila siku na RAI kila Alhamisi ya wiki kuwa, gazeti lililowekwa kwenye mitandao ya
kijamii si gazeti halisi la RAI wala habari zile hazijawahi kuandikwa na RAI hata mara moja.

“Na hata ukizisoma habari zilizomo kwenye gazeti linalosambazwa mtandaoni zimetawaliwa na dhamira ya
kulipaka matope gazeti halisi la RAI, wahariri na waandishi wake kwa malengo ambayo hatujayajua.

“Katika uchunguzi wetu tuliofanya baada ya gazeti feki kuwekwa mitandaoni kwa mara kwanza, tuliona kazi hiyo haramu inafanywa katika chumba kimoja cha habari ambacho watendaji na wahariri wake wana mrengo fulani wa kihabari.

Tulikaa kimya wakati ule wa kwanza kwa maana tuliamini wangejifunza kutokana na upuuzi wao.
“Lakini baada ya kuona wamerudia, tumeona kuna wajibu wa kuwajulisha wasomaji wetu ambao baadhi wanaingia kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kusoma magazeti, kwamba kile ambacho wanakiona kwenye mitandao si magazeti halisi ya MTANZANIA na RAI.

“Kutokana na hali hiyo, tunaangalia namna bora ya kuwasiliana na mamlaka husika za kiserikali ili kupata njia sahihi ya kuwashughulikia hawa wanaokiuka sheria ya mitandao,” alisema. Kibanda, amewataka watu hao wenye nia ovu na Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuachana na mikakati yao hiyo miovu kwani haitawasaidia kufanikisha malengo yao dhalimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles