BRIGHITER MASAKI
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na Mkurugenzi wa Rockstar, Ali Kiba, amefanikiwa kupata mtoto wa kiume na mkewe aliyefunga naye ndoa mapema mwaka jana.
Mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Kadogo, amethibitisha kupata mtoto kupitia Snapchat kwa kuweka picha ya mguu na mkono wa mtoto.
Baada ya muda, msanii huyo aliposti video fupi ikiwaonyesha watoto wakituma salamu kwa msanii huyo wakimwambia hongera kwa kupata mtoto wa kiume.
“Hongera kwa kupata mtoto wa kiume na mlinde mtoto kwa ajili yetu,” walisema watoto hao kupitia video hiyo.
Huyo ni mtoto wa kwanza kwa Ali Kiba na mkewe, lakini staa huyo tayari alikuwa na mtoto.