29.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 30, 2024

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Fatma Karume njia panda urais TLS?

MWANDISHI WETU

RAIS wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika( TLS), Fatma Karume ambaye anamaliza muda wake Aprili mwaka huu, anaonekana kuwa njia panda kuchuka uamuzi wa kutetea kiti chake au la.

Mazingira hayo yanajidhihirisha kwa  ukimya mkubwa alionao katika kipindi hiki cha kuomba nafasi za uongozi wa chama hicho ambacho kinafikia tamati 11 jioni  Jumatano ya wiki ijayo.

Ukimya huo wa Fatma pia unatajwa kuwaweka  njia panda zaidi  baadhi ya wanachama wa TLS hasa wale waliokuwa na matumaini ya kuona kiongozi huyo anatetea kiti chake.

Licha ya kamati ya uchaguzi ya chama hicho Februari 13 mwaka huu kutangaza kuwa imesogeza mbele zoezi la kupokea maombi ya wagombea hadi  Jumatano wiki ijayo, lakini Fatma bado hajajitokeza kuonyesha nia ya kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

MTANZANIA Jumapili ndani ya wiki hii  lilikuwa kwenye jitihada za kumtafuta Fatma ili aelezee msimamo wake juu ya uchaguzi wa mwaka huu, lakini hakupokea simu kila alipopigiwa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi kupitia katika mtandao wa Whatsapp  hakujibu.

Gazeti hili halikukomea hapo tu, lilimuuliza

Hata hivyo jana katika akaunti yake ya twitter yenye utambulisho wa jina la fatma karume a.k.a Shangazi aliandika ujumbe uliosomeka “ Good morning everyone . Najua nilikuwa kimya kwa muda. Don’t worry hawajaniteka ili nikae kimya, niko busy kidogo.” 

Kabla ya Fatma kuandika ujumbe huo jana, gazeti hili lilimtafuta  Wakili Peter Kibatala ambaye aliongoza timu ya kampeni za Fatma katika uchaguzi wa mwaka jana ili aeleze kama kiongozi huyo atatetea kiti chake lakini Kibatala hakupokea simu kwa siku mbili mfululizo na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maelezo hakujibu.

Mbali na Kibatala gazeti hili lilimuuliza  Makamu Rais wa TLS Dk Rugemeleza Nshala anafahamu chochote juu ya Fatma kutetea kiti chake ambapo alijibu kwamba hafahamu.

Alipoulizwa anauchukuliaje ukimya wa Fatma hasa katika hiki cha mwisho mwisho kuelekea tamati ya kuwasilisha maombi ya kugombea nyadhifa ndani ya chama hicho, Dk. Shala alisema labda bado anajitafakari kwa sababu muda bado upo.

“ Sijui kama Fatma anauamuzi wa kutotetea kiti chake au la lakini ninachoamini ni kwamba mpaka tarehe 20 ni siku nyingi, inawezekana kabisa bado anafikiria kwa hiyo tusubiri mpaka siku ya mwisho ya uwasilishwaji wa maombi,” alisema Dk. Nshala.

Katika uchaguzi wa mwaka jana Fatma alijitokeza katika dakika za mwisho mwisho kuwania urais wa TLS  na kufanikiwa upepo wa uchaguzi huo kwa kuonekana na ni mtu sahihi wa kumrithi Tundu Lissu ambaye alikuwa anamaliza muda wake.

 Fatma alichuana na kufanikiwa kuwabwaga  Godwin Mwapongo, Godfrey Wasonga na Godwin Ngwilimi ambao tayari walikuwa wameonyesha kuwa na ushawishi mkubwa wa kuchaguliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles