25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Sekondari Lindi yaanzisha mpango kuinua ufaulu kwa wanafunzi wa kike

Hadija Omary, Lindi

Shule ya Sekondari Kitomanga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, imeandaa mpango maalumu wa kuwasaidia wanafunzi wa kike kufanya vizuri katika masomo yao ili kuinua kiwango chao cha ufaulu mkoani humo.

Akizungumza na Mtanzania Digital mwishoni mwa wiki Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Patrick Mwankenda, amesema kuwa mpango huo umepewa jina la Girls Education Supports  ambao utajikita zaidi katika kuwajenga watoto wa kike kupenda masomo ya Sayansi.

Amesema lengo kuu la kuanzisha mpango huo ni kuleta mwamko wa elimu kwa watoto wa kike na kuleta hamasa kwa watoto wa kike kupenda kusoma masomo ya sayansi ambayo mwamko wake kwa wanafunzio wa kike mkoani humo bado mdogo.

“Hali hiyo inajidhihirisha hata katika mitihani inayotolewa shuleni ukilinganisha na watoto wa wa kiume ambao hufaulu zaidi masomo hayo kuliko wa kike.

“Uendeshaji wa mpango huu utakuwa ni shirikishi ambapo utaendeshwa kwa kufanya mitihani ya kujipima kwa kushirikiana na shule za jirani, darasa moja na darasa jingine na midahalo,” amesema.

Katika midahalo, amesema mbinu watakayotumia ni kualika wanawake wamefanikiwa kwa kuwatumia wataalamu kutoka idara mbalimbali kama vile mainjinia, madaktari na wengine ili watoe elimu ya namna gani watoto hao wa kike wanaweza kufikia malengo yao kama wao.

“Mpango huo utakuwa endelevu ambapo matarajio yetu ni kuinua ufaulu wa watoto wa kike katika shule yetu na shule jirani, pamoja na kuhakikisha mwanafunzi anayeanza kidato cha kwanza anamaliza kidato cha nne,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles