Jenerali Mabeyo atinga Njombe, atoa kauli mauaji ya watoto

0
1176

Elizabeth Kilindi, Njombe

Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo, ametinga mkoani Njombe kutokana na mauaji ya watoto yanayoendelea mkoani humo ambapo amesema watakomesha mauaji hayo yanayosababishwa na imani potofu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari 11, mara baada ya kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa, amesema sasa jeshi linataka kuzitoa imani potofu kwa wananchi na kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida.

“Tutakomesha mauaji haya nchi nzima si Njombe peke yake, tunawaomba watu waendelee na kazi zao kama kawaida vyombo vya usalama viko tayari kufanya kazi mchana na usiku,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here