KUALA LUMPUR, Malaysia
MFALME wa hapa, Muhammad V ametangaza kujiuzulu wadhifa wake ikiwa ni mara ya kwanza tukio hilo kutokea kwa kiongozi kama huyo kuachia madaraka kabla hajamaliza kipindi cha miaka mitano ya utawala wake.
Taarifa ya mfalme huyo kujiuzulu ilitolewa jana na kasri ya kiongozi huyo, lakini haikutaja sababu za kujiuzulu na huku maofisa wa ofisi wakishindwa kutoa majibu.
Baraza la kifalme la hapa lina wafalme tisa na mrithi wa kio ngozi huyo anaweza kuchaguliwa na viongozi hao.
Katika taarifa hiyo ya Kasri ilieleza kuwa mflame huyo anasema kwamba anapongeza kwa nafasi hiyo aliyokuwa amerpewa na akawashukuru Waziri Mkuu na Serikali yake.
“Kwa upeo wake umefanya kazi ili kutekeleza majukumu yake aliyopewa na mkuu wa serikali, akiwa kama nguzo ya utulivu, chanzo cha haki, msingi wa umoja kwa ajili ya watu wote wa taifa hili,” taarifa hiyo ya kifalme ilieleza bila kutaja sababu za kuachia kwake madaraka..
Hata hivyo kujiuzu kwa mfalme huyo kumekuja ikiwa ni takribani wiki moja tangu aanze kazi, baada ya kutumia muda wa miezi miwili akiwa nje ya nchi kwa ajili ya likizo ya matibabu.