30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake nchini Saudia kupewa talaka kupitia ujumbe wa simu

RIYADH,Saud Arabia

SHERIA   mpya nchini hapa  inawalinda wanawake kutopewa talaka bila kujua na hivyo kuanzia  jana  mahakama zitatakiwa kuwaelezea wanawake kupitia njia ya ujumbe wa simu kwamba wamepewa talaka.

Mawakili wanawake waliosimamia sheria hiyo wanapendekeza kuwa hatua hiyo itamaliza kile kinachotajwa kuwa talaka za siri  ambapo wanaume hutoa talaka bila kuwaelezea wake zao.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, agizo hilo litahakikisha kuwa wanawake wanajua hali ya ndoa zao na itawalinda dhidi ya maslahi yao..

Mwaka uliopita marufuku ya wanawake kuendesha magari iliondolewa na mahakama nchini  hapa, lakini hata hivyo wanawake bado wako chini ya usimamizi wa wanaume.

”Sheria hiyo mpya itahakikisha kuwa wanawake wanapewa haki zao za masurufu wakati wanapopewa talaka”, alisema Wakili Nisreen al-Ghamdi.

Alisema kwamba pia itahakikisha kuwa uwezo wowote utakaotolewa na mahakama hautumiki vibaya.

”Wanawake wengi wamewasilisha malalamisihi yao katika mahakama za rufaa kwa kupewa talaka bila ya wao kujua” , alisema wakili mwingine,  Samia al-Hindi.

Hatua hiyo mpya inasemaekana kuwa miongoni mwa mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yalioshinikizwa na mwanamfalme Mohammed bin Salman, ikiwemo kuwaruhusu wanawake kuingia uwanjani na kutazama mechi za mpira wa miguu.

 Kuna vitu vingi ambavyo wanawake wa Saudia bado hawaruhusiwi kufanya bila ya kuomba ruhusa kutoka kwa wasimamizi wao kama vile waume zao , baba zao ndugu wa kiume ama watoto wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles