32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Jeshi la Polisi laanika mbinu kukabili ajali za viongozi

VERONICA ROMWALD, DODOMA

ILI kudhibiti wimbi la ajali za barabarani zikiwamo zinazohusisha gari za viongozi na watumishi wa umma, Jeshi la Polisi jijini hapa limeeleza mikakati yake ikiwamo kuwapa mafunzo ya muda mfupi.

Hayo yalielezwa jijini hapa jana na Kamanda wa Polisi Dodoma, Gilles Muroto, ofisini kwake alipozungumza na waandishi wa habari walio katika mradi wa usalama barabarani unaosimamiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kikosi cha Usalama Barabarani, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

“Dodoma ni mji mkuu na makao makuu ya nchi, viongozi wengi wa Serikali wamehamia hapa akiwamo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na wakuu mbalimbali wa nchi.

“Shughuli nyingi za kitaifa zinafanyika hapa, kwa msingi huo tunahakikisha tunaimarisha usalama kila kona hadi huko barabarani, wanakuja salama na kuondoka salama, hakuna ajali,” alisema.

Alisema ili kuhakikisha madereva wa viongozi na watumishi wa umma wanaendelea kuendesha kwa usalama wanawapa mafunzo ya miezi mitatu.

“Hivi karibuni kulikuwa na changamoto ya ajali, tumechukua hatua, tunawaita, wanakaa kwenye bwalo letu pale tunawafundisha, lengo ni kuwakumbusha maana mtu anaweza kuwa amepata leseni muda mrefu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles