29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli aibuka na pushapu

g2*Asema ana nguvu ya kuleta mabadiliko ya kweli

Na Bakari Kimwanga, Karagwe

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, ametoa mpya baada ya kuibuka na staili mpya ya kuomba kura kwa mtindo wa kupiga pushapu akiwa jukwaani.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuomba kura, huku akisema ana nguvu za kuwatumikia kwa dhati na kuomba aoneshe jukwaani kama ana nguvu kweli.

Dk. Magufuli aliibuka na mtindo huo jana katika mkutano wake wa pili wa kampeni mjini Kagarwe mkoani Kagera.

Hii ni mara ya kwanza katika siasa za Tanzania, mgombea urais kupiga pushapu jukwaani tangu mfumo wa vyama vingi urejee nchini mwaka 1992.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika wilaya za Misenyi, Karagwe, Kyerwa na Ngara, Dk. Magufuli alisema nguvu na afya aliyonayo ndivyo vinavyompa jeuri ya kuomba kuwatumikia Watanzania.

“Nipo tayari hata kurukaruka (anaruka), kwa lolote au hata kupiga pushapu hapa ninaweza au mnataka nipige?” alihoji na wananchi wakaitikia kwa sauti kubwa. “Ndiyooo”.

Baada ya wananchi kuitikia, Dk. Magufuli akiwa ameshika kipaza sauti alianza kupiga pushapu hadi zilipofika tano akasimama.

Kitendo hicho kiliamsha shangwe kwa wananchi ambao walimshangilia na wengine wakiangua vicheko.

Dk. Magufuli, alisema anaomba urais na amedhamiria kuboresha huduma bora na nzuri za jamii hasa katika sekta ya maji, elimu na barabara.

Alisema anashangazwa kuibuka matapeli wa kisiasa ambao wamekuwa wakiwalaghai wananchi kwa mambo ambayo hawawezi kuyatekeleza hata kama watapewa urais.

“Ninaomba urais kutaka kushughulika na matapeli wa kisiasa. Lazima Watanzania tuwaambie ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

“Nataka tuwe na Tanzania yenye mabadiliko ili tuweze kuondoa umaskini kwa wananchi na pamoja na kuimarisha soko la kahawa,” alisema Dk. Magufuli

Alisema moja ya mikakati yake ya Serikali ya awamu ya tano, ni kuhakikisha inapandisha soko la uhakika kwa kahawa inayozalishwa nchini.

“Serikali ya Magufuli, itahakikisha kahawa yetu tunapandisha soko lake kwa kuondoa kodi 26 ambazo zimekuwa zikiwanyonya wakulima.

“Tutakachokifanya ni kujenga kiwanda ambacho kitasaga hapa na tutauza kahawa ikiwa tayari, badala ya kuuza kahawa ghafi nje nchi.

Alisema akiwa waziri wa ujenzi, ameweza kusimamia ujenzi wa barabara ya lami kutoka Bukoba hadi Karagwe, huku akiahidi kumalizia kilometa 100 zilizobaki.

“Ninapenda kuambia pamoja na baadhi ya watu kusema hakuna kilichofanyika katika miaka 54 ya utawala wa CCM, hawaioni tena wengine walikuwapo humuhumu na anasema walipeleka maji Shinyanga basi hakuna walichofanya.

“Leo mtu unatoka Karagwe hadi Dar es Salaam kote lami, tumebakiza eneo dogo ambalo tutaweka mpaka Benako,” alisema

 

Lukuvi

Akiwa wilayani Misenyi katika Jimbola Nkenge ambalo linawaniwa na Balozi Dk. Diorous Kamala, Magufuli aliahidi kushughulikia kilio cha wananchi ambao maeneo yao yamechukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Omkajunguti.

Alisema anatambua kazi kubwa inayofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

“Ninasema fidia lazima ilipwe kwa wananchi, ninataka kuwaambia  kwa mujibu wa sheria namba 4 ya Ardhi ya mwaka 1999  na ile ya matumizi bora ya ardhi, lazima fidia ije.

“Nawahakikishia itasimamiwa na Waziri Lukuvi (William), mwenyewe ni waziri mzuri sana anafanya kazi nzuri sana,” alisema.

Alisema kama atachaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataondoa vizuizi vilivyowekwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Hili la wingi wa vizuizi tutaliangalia na ikiwa mtanipa ridhaa nitaviondoa, haiwezekani Watanzania wapate kero ya vizuizi katika nchi yao,” alisema.

 

Kiwanda cha bati

Alisema anajua Wilaya ya Kyerwa, ina rasilimali nyingi ikiwemo madini ya kutengeneza mabati.

Alisema Serikali yake, itakuwa ya viwanda huku akiahidi kujenga kiwanda cha mabati ambacho kitasaidia kutoa ajira kwa vijana pamoja na kujenga nyumba kwa gharama nafuu.

“Kyerwa ni wilaya mpya lakini hakuna asiyejua kuwa hapa kuna madini ya chuma cha kutengeneza mabati, sasa tutajenga kiwanda hapa badala ya kusubiri kununua mabati kutoka Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles