29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara wajazwa mamilioni kwa kufanya miamala

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Selcom kwa kushirikiana na Mastercard imetoa zawadi ya Sh milioni tatu kwa wafanyabiashara wanaotumia huduma ya Masterpass QR katika kupokea malipo mbalimbali kwenye maeneo yao ya biashara.

Zawadi hizo zimetolewa jana katika promosheni ya ‘Shinda Mtaji’ iliyoanza rasmi Novemba mwaka huu kwa lengo la kuwarahisishia wafanyabiashara hao kutumia huduma ya Masterpass QR kufanya miamala mbalimbali.

Akizungumza promosheni hiyo, Meneja Masoko wa Selcom, Juma Mgori alisema promosheni hii inamuwezesha mfanyabiashara kujishindia Sh milioni moja kila wiki kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Novemba mwaka huu hadi Januari mwaka 2019.

Aidha, aliwataja wateja walioshinda milioni moja kila mmoja kuwa ni Boaz Wales, Hamisi Kilenga wote wa mkoani Dar es Salaam na mfanyabiashara mmoja kutoka Arusha.

Alisema kila mfanyabiashara atakayejiunga na Masterpass QR na kuanza kupokea miamala kutoka kwa wateja, ataingia moja kwa moja kwenye droo ya promosheni kwa wiki hiyo na kupata nafasi ya kujishindia hivyo kumuwezesha kujiongezea mtaji wa biashara yake.

“Masterpass QR ni huduma inayomuwezesha mteja kufanya malipo ya bidhaa na huduma mbalimbali kutoka kwenye akaunti ya simu au akaunti ya benki kwa kuingiza Pay Number ya mfanyabiashara au ku-skani kodi ya QR iliyopo kwenye eneo la mfanyabiashara kwa kutumia Smartphone.

Mmoja wa washindi hao Boazi Walesi alisema huduma ya Masterpass QR imemwezesha kuwaondoa adha ya kubeba fedha taslimu au kuwa na kadi ya benki muda wowote wanapohitaji kufanya malipo.

Naye Hamisi Kitenga alisema mfanyabiashara anapojiunga kutumia huduma hiyo fedha za mauzo ya siku zitatumwa kwenye akaunti yake ya benki au simu siku hiyo hiyo baada ya siku ya kazi kuisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles