32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Mawasiliano yaagiza mafundi simu wasajiliwe

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeiagiza Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kusajili mafundi wanaotoa huduma za matengenezo ya simu za mkononi kwa mujibu wa sheria zilizopo na kuhakikisha huduma wanaozotoa kwa wananchi zina viwango stahiki.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Sekta ya Mawasiliano Dk Jim Yonaz leo Jumatano Disemba 5, alipokuwa akiwatunuku vyeti vya kuhitimu mafunzo ya miezi mitano kwa mafundi simu 68 yaliyotolewa katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia (DIT).

Dk Yonaz amewataka mafundi simu hao kutumia elimu waliyoipata katika mafunzo hayo wakaitumie kwa kuwahudumia wananchi kwa uadilifu mkubwa na kuwa mfano kwa mafundi wa aina hiyo hapa nchini.

“Kuanzisha mafunzo haya ya kurasimisha ufundi wa simu za mkononi kutawasaidia mafundi kufanya kazi kwa weledi na ufahamu lakini pia itaisaidia TCRA kutoa leseni kwa mafundi ambao kiwango chao kinafahamika.

“Yamekuja kwa wakati muafaka na naomba yaendelee kusimamiwa vyema ili mafundi simu za mikononi nchini kote waweze kupata elimu hii, ” amesema Dk Yonaz.

Aidha Dk Yonaz ametoa rai kwa wadau wa Mawasiliano nchini kubuni mipango endelevu ya kushirikiana kuchangia katika kufanikisha mafunzo hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles