27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Marafiki wa Dk. Tulia watoa msaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Derick Milton, Simiyu

Umoja wa Marafiki wa Dk. Tulia Ackson Mkoa wa Simiyu (Friends of Dk.Tulia), wametoa msaada wa madaftari, nguo, viatu, na vifaa vingine vya kujifunzia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi Sima ‘A’ iliyoko Halmashauri ya Mji wa Bariadi, vyenye thamani ya Sh milioni mbili.

Akiongoza umoja huo, Mwenyekiti wa Friends Of Dk. Tulia, Matiko Nyaiho, amesema wametoa msaada huo ikiwa sehemu ya kushiriki kampeni ya siku 16 za kupiga vita ukatili wa kijinsia.

Mbali na msaada huo, umoja huo kwa kushirikiana na jeshi la polisi dawati la jinsia, wametoa elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo juu ya kupiga vita ukatili wa kijinsia pamoja na mimba za utotoni.

“Msaada huu umelenga kumsaidia kiongozi wetu (Dk. Tulia) katika masuala ya kijamii zaidi, ndiyo maana tumeutoa kwa watoto wenye mahitaji maalumu kutokana na kuishi katika mazingira magumu na kukabiliwa na changamoto nyingi,” amesema.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Pendo Ntale ameshukuru Umoja huo kwa kuleta msaada kwa wanafunzi hao, huku akieleza kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya mavazi na chakula.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,451FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles