25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi wawadai madereva

FERDNANDA MBAMILA NAJOHN KIMWERI (DSJ) DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi linadai zaidi ya Sh bilioni 16 kwa madreva mbalimbali ambao wameandikiwa faini kutokana na makosa mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha jeshi hilo, Ahmed Msangi, alisema kati ya madeni hayo faini za ndani ya siku saba ni Sh milioni 812.88.

Alisema madeni yaliyokaa kwa zaidi ya siku saba ni Sh bilioni 15.307.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko ya kawaida ambapo aliyekua msemaji wake, Barnabas Mwakalukwa amehamishiwa Mkoa wa Pwani kuwa Mnadhimu, huku nafasi yake ikichukuliwa na Msangi.

Kwa mujibu wa Msangi mabadiliko hayo yaliyofanyika siku tatu zilizopita yamelenga kuboresha utendaji kazi wa jeshi hilo.

“Lengo kuu la mabadiliko hayo ni kufanya kazi kwa kulitumikia Jeshi la Polisi ili kuimarisha ulinzi na usalama,”alisema.

Alisema hali ya usalama nchini ni shwari licha ya changamoto za uhalifu mdogomdogo unaoendelea kutokea nchini.

“Tumeendelea kukabiliana nao kadri ya uwezo wetu, kwa hili niwashukuru wananchi hasa raia wema ambao wamekuwa wakitupatia taarifa zinazowezesha kuzuia uhalifu kabla haujatokea,” alisema. Alisema takwimu zinaonyesha kuwa makosa ya jinai yaliyoripotiwa kwa kipindi cha Januari hadi Oktoba 2017 yalikuwa 496,677 ikilinganishwa na makosa ya jinai 489,429 yaliyoripotiwa katika kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka 2018.

Kwa kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka 2018 makosa dhidi ya binadamu yaliyoripotiwa yalikuwa 9,745 ikilinganishwa na makosa 10,567 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2017.

Aliyataja kwa mfano makosa ya mauaji yamepungua kutoka makosa 2,538 yaliyo ripotiwa katika kipindi cha Januari hadi Oktoba 2017 hadi makosa 2209 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2017.

Makosa ya barabarani katika kipindi cha Januari hadi Oktoba 2018 yalikuwa 3,419 ikilinganishwa na matukio ya ajali 5,073, yaliyopitiwa katika kipindi cha mwaka 2017 ambayo ni pungufu wa matukio 1,654 sawa na asilimia 32.6.

“Matukio ya ajali zilizosababisha vifo yamepungua kutoka matukio 1,887kwa kipindi cha januari hadi oktoba 2017 hadi matukio 1,264 kwa kipindi kama hicho kwa mwaka 2018 ikiwa ni upungufu wa matukio 623 sawana asilimia 33.

Alisema ajali zilizosababisha vifo kulisaidia pia kupungua kwa idadi ya watu waliopoteza maisha kwa ajali za barabarani ambapo katika kipindi cha Januari hadi Oktoba 2018, kuliripotiwa vifo vya watu 1661 ikilinganishwa na idadi ya watu 2,250 waliopoteza maisha katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2017 ikiwa na upungufu wa vifo 589 sawa na asilimia 26.2

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles