29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima wa korosho wavuna bilioni 40

MATHIAS CANAL, MTWARA

WAKULIMA 40,208 wa zao la korosho katika mikoa ya kusini hadi sasa wamekwishalipwa Sh bilioni 41.8.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, ambapo hadi juzi uhakiki ulifanywa kwa vyama 220 vya korosho kati ya 504 vilivyopo Mtwara, Lindi na Ruvuma.

Akizungumza kwenye kikao kazi cha Watendaji wa timu ya Oparesheni korosho kilichofanyi­ka katika ukumbi wa CBT mkoani Lindi, Hasunga alisema kati ya vyama hivyo vilivyohakikiwa 181 tayari vimelipwa.

Aliongeza kuwa wakati zoezi hilo linaanza Serikali ilikuwa inali­pa Sh bilioni moja kwa siku lakini kwa sasa utaratibu uliowekwa ni kulipa kati ya Sh bilioni 5 mpaka 10 kwa siku.

Hasunga aliongeza kuwa Seri­kali imeamua kuwalipa wabebaji na wapakiaji wa mizigo kwenye maghala sambamba na kuanza kuwalipa malipo ya awali wasa­firishaji kutoka kwenye vyama vya msingi kwenda kwenye vyama vikuu.

Kuhusu suala la magunia, Hasunga alisema Serikali im­eamua kuyalipa magunia yote ili kurahisisha uhifadhi wa korosho.

Katika hatua nyingine, Hasun­ga alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe kumsimami­sha kazi mtumishi George Mboje na kumwondoa kwenye timu ya Operesheni Korosho.

Pamoja na kumwondoa kwenye timu hiyo pia Katibu Mkuu ametakiwa kumwondoa kwenye Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko.

“Katibu Mkuu, nataka umuon­doe huyu George kwenye hii timu na pia sitaki kumwona kwenye Bodi na Taasisi yoyote katika Wiz­ara ya Kilimo” alisisitiza Hasunga.

George Mboja ambaye yupo kwenye timu ya Oparesheni Korosho akiwakilisha Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko anatuhumiwa kwa utovu wa nidhamu sambamba na kushind­wa kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wa Oparesheni Korosho inayoendelea nchini.

Aidha, Waziri Hasunga amewahakikishia watendaji hao kuwa serikali ina fedha za kutosha kuwalipa wakulima wa korosho lakini lazima wakulima wote wahakikiwe ili kujiridhisha kwamba anayelipwa ni mkulima wa mwisho na si wafanyabiashara maarufu kama Kangomba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles