26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Samia: Hatuwapi wapinzani nchi

Pg 2 sept 22NA SARAH MOSSI, MKINGA

MGOMBEA mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, amesema chama hicho hakiwezi kutoa nchi kwa chama cha upinzani ambacho hakijajipanga.

Samia, alisema hayo jana wilayani hapa wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Duga Maforoni na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC), Mahadhi Juma Maalim.

Alisema wapinzani hawakujipanga kuongoza nchi, na kwamba hata wakati wanazindua ilani yao ya uchaguzi, waliwataka wananchi wakasome kwenye tovuti.

“Tumejipanga tunajuana, nani anatoka wapi, wagombea wao ni wa kuchangachanga. Hata akija mtu kumposa mwanao unaangalia katoka wapi, ukoo upi, ana matatizo gani,” alisema.

Samia aliwaahidi wananchi wa Mkinga kuwa Serikali imejipanga kuyafanyia kazi madai yao ya fidia, baada ya kupisha ujenzi wa barabara kutoka Tanga kwenda Horohoro.

Hata hivyo, aliwataka wananchi hao kuendeleza zao la korosho ambalo wameliacha na kusisitiza Serikali ya Norway imeahidi kujenga viwanda vitatu vya kubangua korosho wilayani Mkinga.

“Limeni korosho ili viwanda vya kubangua korosho vipate kufanya kazi, nawasihi  fanyeni kazi ya kulima zao hili, viwanda vinakuja,” alisema Samia.

Akizungumzia tatizo la watoto wa kike kuacha shule kutokana na mimba, Samia aliahidi Serikali itajenga mabweni ili kunusuru watoto wa kike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles