26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mgombea apigwa, gari lake lavunjwa vioo

RPCNa Walter Mguluchuma, Katavi

ZIKIWA zimesalia siku 32 kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, mgombea ubunge Jimbo la Mpanda Vijijini, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mussa Kantambi, amepata kipigo kutoka kwa wafusi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na MTANZANIA mjini Mpanda jana, Kantambi  alisema alipigwa vibaya, huku gari lake likivunjwa kioo cha mbele baada ya kupita eneo ambalo CCM walikuwa wakifanya mkutano.

Alisema tukio hilo, lilitokea juzi saa 6 mchana katika eneo la Santamaria, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, akiwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili T 390 ANM.

“Nilikuwa natoka Mpanda Mjini nakwenda Kijiji cha Kabage kufanya mkutano wa kampeni, sasa wakati nafika pale, nilikuta barabara imefungwa, ilibidi nisimame kwa ajili ya kutafuta sehemu ya kugeuza gari.

“Wakati natafuta sehemu ya kutokea, pale nilimkuta mgombea ubunge wa Jimbo la  Mpanda Mjini, Sebastiani Kapufi (CCM) anaendelea na mkutano wake wa kampeni, lakini ghafla wafuasi wake walihamaki na kuanza kunishambulia.

“Sikuwa na nia mbaya, nilikuwa natafuta pakutokea, ghafla nilianza kupigwa mawe kila kona na wana CCM,” alisema.

Alisema baada ya kushambuliwa, aliamua kujiokoa kwa kukimbilia kwenye nyumba ya mtu na kutelekeza gari lake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alikiri kuwapo tykio hilo.

“Kweli tukio hili lilitokea pale Santamaria, Mtaa wa Mwamkulu, gari la mgombea wa Chadema lilishambuliwa kwa mawe na kuvunjwa vioo,” alisema.

Alisema hakuna mtu aliyekamatwa baada ya wagombea hao kukutana na kukubaliana kumaliza tatizo wenyewe.

Kamanda Kidavashari alisema Jeshi la Polisi mkoani hapa, limeandaa mkutano Septemba 25, mwaka huu ambao utahusisha viongozi wa madhehebu yote ya dini, vyama vya siasa na wazee mashuhuri.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles