27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Lowassa: Msiiogope Serikali kuchangia

edoloNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, amewataka Watanzania kumchangia bila hofu ya kutishwa na Serikali.

Lowassa, alitoa wito hu jijini Dar es Salaam juzi kwenye mkutano wa harambee ya kuchangia fedha za kusaidia ndoto ya mabadiliko.

Katika harambee hiyo, jumla ya Sh milioni 80 zilikusanywa zikiwamo fedha taslimu na ahadi, ambapo fedha taslimu zilipatikana Sh milioni 9.5, huku wafuasi wa chama hicho nje ya nchi walichangia dola za Marekani 500 na hundi ya Sh milioni moja.

“Kuna watu wanaogopa kuchangia kwa sababu wanafuatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wako wengine wanaofuatwa na viongozi wa Serikali.

“Nawaomba msiogope hata kidogo, hawana haki ya kuwafuata wala haki ya kuwahoji, suala la mabadiliko linahusu kila mtu, halichagui aliyechangia, asiyeyachangia, anayewapenda waleta mabadiliko au asiyewapenda. Lakini yanapofanyika hufanyika kwa faida ya nchi,” alisema Lowassa.

 

MBOWE

Naye Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema harambee inayofanywa na Ukawa haina faida kwa Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi, NLD au Chadema, bali inasaidia maisha ya baadaye ya watoto.

“Kila mmoja achange kwa uwezo wake, na kwa bahati mbaya sisi wapinzani hatuna fedha hizo ambazo wenzetu wanasema kwamba tuna fedha nyingi, bali tumekuwa tunakijenga chama hiki kwa kujitolea, hata vyombo vya usafiri tunavyotumia huwa watu wanajitolea,” alisema Mbowe.

Mwenyekiti huyo alisema umoja huo umepanga kutafuta fedha hizo ili kusaidia gharama za siku 34 za kampeni zilizobaki za kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumzia kuhusu namna wanavyoendesha kampeni, Mbowe alisema kuwa wamekuwa wakiziendesha kistaarabu kama walivyokuwa wameahidi hapo awali.

“Pamoja na CCM kutoendesha kampeni za kistaarabu kwa wagombea wao, lakini sisi tumeendelea kuendesha kampeni za kistaarabu bila kujali tunavyoonewa sana, kutukanwa. Lakini sisi tumevumilia ili kufikia mabadiliko,” alisema Mbowe.

Alisema haitakuwa rahisi kufanya mabadiliko kwa taifa lililojaa hofu ya kuhofia kufuatwa pindi watakapoonekana wamechangia mabadiliko kusonga mbele.

“Kuna watu wanasema wanapenda kutuchangia, lakini wakija kwenye harambee au kutumia simu wataona namba zao, bado wapo watu wanahofu, hatuwezi kufanya mabadiliko.

“Fedha zako, tena za halali unaogopa kuchangia mabadiliko, eti unaogopa watu wa Serikali ambao wengi wao ni wezi na mafisadi, lakini unawaogopa. Napenda kuwaambia kwamba mabadiliko yanaweza kuja kwa fedha au bila fedha,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles