25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Ukraine yatangaza hali ya hatari kwa kuihofia Urusi

KIEV, Ukraine



SERIKALI ya hapa  imetangaza hali ya hatari  kwa siku 30 katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo ambazo zinakabiliwa na vitisho vya kushambuliwa na Urusi.

Akitangaza hatua hiyo, Rais Petro Poroshenko alisema sheria hiyo ni muhimu   kuimarisha ulinzi wa nchi  baada ya Urusi kukamata meli tatu za wanamaji    karibu na eneo la Crimea na kuwashikilia mateka mabaharia wake.

Hatua hiyo inaonekana kumkera hata Rais wa Marekani,  Donald Trump aliyesema jana kwamba hapendi hali inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine na kuwa anashauriana na viongozi wa Ulaya kuhusu suala hilo.

Katika kikao cha dharura cha Bazara la Usalama la Umoja wa Mataifa, Balozi wa Marekani, Nikki Haley alionya Urusi kuwa kitendo chake cha kuzikamata meli hizo ni ukiukaji mkubwa wa uhuru wa mipaka ya Ukraine.

Hata hivyo Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, Dmitry Polyasnkiy aliituhumu Ukraine kwa kupanga tukio hilo kama njia ya kuimarisha umaarufu wa Poroshenko kabla ya uchaguzi wa Machi.

Umoja wa Ulaya, Uingereza, Ufaransa, Poland, Denmark na Canada zote zimelaani kile zilichoema  uchokozi wa Urusi.

Kiongozi wa Ujerumani Kansela Angela Merkel amesisitiza haja ya kufanyika mazungumzo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles