33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Hofu ya volcano yatanda Mlima Meru

IMG-20150920-WA0013NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

WAKAZI wa Jiji la Arusha jana walikumbwa na hofu kubwa, baada ya kitu kinachosadikiwa kuwa ni volcano kulipuka Mlima Meru.

Hali hiyo ilisababisha wingu zito la vumbi kutanda angani huku wakazi wa vijiji vinavyozunguka mlima wakikimbia maeneo yao. Wingu hilo lililotanda angani lilianza kuonekana saa 9 alasiri upande wa Kaskazini mwa Mlima Meru kisha kuendelea kusambaa hadi juu ya kilele cha mlima huo.

MTANZANIA lilishuhudia vumbi hilo likielekea upande wa Kaskazini mwa Jiji la Arusha kutokana na upepo uliokuwa ukivuma. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa jijini hapa jana walionyesha wasiwasi na kudai hawajawahi kuona vumbi zito likifunika mlima wote. Kwa upande wake mkazi wa Mianzini, Edward John, aliyeishuhudia hali hiyo alisema inawezekana zikawadalili za kulipuka volcano.

“Najisikia kuvuta hewa nyepesi kifuani kama harufu ya saruji, vumbi linalotoka Mlima Meru,” alisema mkazi wa
eneo la Kaloleni, Lazaro Mtei.Vyanzo vya kutoka vijiji vya Kisimiri Juu na Ngarenanyuki, vilidai haikuwa volcano
kama ilivyohofiwa na watu wengi bali ni moto ulioanza kuwaka kwenye hifadhi ya mlima huo tangu juzi. Juhudi za
gazeti hili kupata mamlaka za hifadhi za mlima huo ziligonga mwamba kutokana na wengi wao simu zao za kiganjani kutokuwa hewani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles