27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Urusi yateka meli  za kivita za Ukraine

MOSCOW, URUSI

Urusi imeziteka meli tatu za kivita za Ukraine zilizokuwa baharini katika rasi ya Crimea jambo ambalo limeongeza chuki baina ya mataifa hayo mawili.

Kwa mujibu wa Jeshi la wanamaji la Ukrane, meli mbili ndogo za kivita, pamoja na meli moja ya kusindikiza meli ndizo zilizotekwa na wanajeshi wa Urusi na kuwajeruhi wahudumu kadhaa wa meli za Ukraine wamejeruhiwa.

Wakati kila taifa likimlaumu  mwenzake kwa kusababisha kisa hicho, leo hii, wabunge wa Ukraine wanatarajiwa kupiga kura kuidhinisha kuanza kutekelezwa kwa sheria za kijeshi.

Mzozo uliopo ulianza pale Urusi ilipoituhumu Ukraine kwa kuingiza meli katika maeneo yake ya bahari kinyume cha sheria.

Urusi kisha iliweka meli kubwa ya kusafirisha mizigo na kuziba daraja la kuingia kwenye mlango wa bahari wa Kerch, njia pekee ya kuingia kwenye Bahari ya Azov na ambayo hutumiwa na mataifa yote mawili.

Urusi inaituhumu Ukraine kwa kuingia kinyume cha sheria katika maeneo yake ya bahari na usafiri eneo hilo umesitishwa kwa muda usiojulikana kwa sababu za kiusalama.

Ukraine imesema ilikuwa imeifahamisha Urusi kuhusu mpango wake wa kupitisha meli zake eneo hilo kuelekea Mariupol.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles