26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mataruma yatakayojenga reli ya kisasa kuzalishwa nchini

Nora Damian, Pwani



Mataruma milioni 1.2 yatakayotumika katika Reli ya Kisasa (SGR) kwa kipande cha Dar es Salaam – Makutupora yatazalishwa hapa nchini.

Mataruma hayo yanayotengenezwa kwa kutumia kokoto, mchanga, saruji na maji yameanza kuzalishwa katika Kiwanda kilichopo eneo la Soga mkoani Pwani.

Akizungumza jana Novemba 25 wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa reli hiyo, Meneja Mradi (Dar es Salaam – Morogoro), Machibya Masanja, amesema kwa siku kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha mataruma 1,080 na hadi sasa kimezalisha 27,000.

“Watu wamekuwa wakisema tunaagiza mataruma kutoka nje, hapana tunayazalisha hapa hapa kwa kutumia malighafi za viwanda vya ndani na kila taruma lina uzito wa kilo 380,” amesema Masanja.

Amesema kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro wanatarajia kuzalisha mataruma 500,100 na kipande cha Morogoro – Makutupora watazalisha mataruma 703,300.

Kiwanda hicho cha mataruma kimeongeza ajira kwa Watanzania na kama kisingekuwepo fursa hiyo ingeenda nchi za nje.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles