27.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Msemaji wa Serikali: Serikali inasikitishwa kupotea kwa Azory

Mwandishi Wetu, Dare s Salaam

Serikali imesema inasikitishwa na suala la kupotea kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Azory Gwanda, aliyepotea katika maizngira kutatanisha Kibiti, mkoani Pwani.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abasi, amesema hayo jana wakati akitoa mada kwa  wanafunzi wa vitivo mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Tumaini (Tudarco), jijini Dar es Salaam kuhusu Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016.

Akijibu swali la mmoja wa wanafunzi aliyetaka kujua serikali inawahakikishia vipi usalama wanafunzi waandishi wa habari hasa baada ya kutokea masuala kama hayo ya waaandishi wa habari kupotea katika mazingira ya kutatanisha huku akitolea mfano suala la Azory, Dk. Abasi amesema suala la Azory hata serikali inaumizwa nalo.

“Suala la Azory bado serikali inaendelea na juhudi za kumtafuta, lakini huwezi kusema waandishi hawako salama wakati Tanzania pekee tuna waandishi zaidi ya 6,000 na wote wako kazini.

“Kuna waandishi ambao kila siku kazi yao kukosoa serikali katika magazeti yao lakini wapo,” amesema.

Hata hivyo, Dk. Abasi amesema kuna watu wengi wanapotea wakiwamo wakulima lakini si suala ambalo serikali inafurahia na inayafanyia kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles