Mwandishi Wetu, Lindi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kusambaza umeme katika maeneo yote ambayo bado hayajaunganishiwa nishati hiyo nchini yataunganishiwa, ikiwamo na tarafa ya Kilimarondo.
Amesema hayo jana Jumamosi Novemba 17, katika ziara yake mkoani Lindi na kuongeza kuwa Rais John Magufuli anataka kuona kila nyumba ya Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu.
“Serikali imetenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika maeneo yote kwa gharama ya Sh 27,000 pekee.
“Aidha, Serikali haitawajibika tena kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali,” amesema.