25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kourtney, Luka Sabbat ‘wamwagana’

NEW YORK, MAREKANI



       

STAA wa mitindo nchini Marekani, Luka Sabbat, amethibitisha kuachana na mpenzi wake, Kourtney Kardashian, baada ya kunaswa akiwa na mrembo mwingine.

Luka mwenye umri wa miaka 20, alikuwa kwenye uhusiano na mrembo huyo mwenye umri wa miaka 39, lakini Luka mwishoni mwa wiki iliyopita alionekana akiwa na mwanamitindo kutoka nchini Italia.

“Hii inaonesha wazi kuwa, nimefikia mwisho na Kourtney, kila kitu kina mwisho wake na sasa ni wakati wa kila mmoja kufanya mambo yake,” aliandika Luka.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa People, Kourtney Kardashian, amedai alikuwa anaishi na kijana huyo kama sehemu ya kumsaidia aweze kufika mbali na mambo yake, lakini kwa sasa uhusiano wake umefikia mwisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles