30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mtangazaji asota rumande, vyombo vya habari vikionywa Kenya

NAIROBI, KENYA

WASHUKIWA katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara, Monica Kimani, mtangazaji wa televisheni, Jacque Maribe na mchumba wake Joseph Irungu wataendelea kusota rumande hadi Jumatano ijayo wakati ombi lao la dhamana litakaposikilizwa.

Aidha Jaji James Wakiaga anayesikiliza kesi hiyo, amevishukia vyombo vya habari kwa namna vinavyoripoti kesi hiyo.

Jaji Wakiaga ametoa siku saba kwa timu ya waendesha mashitaka kuandaa ripoti kuhusu suala la dhamana na kuipatia timu ya utetezi ifikapo Jumanne ijayo.

Wakili wa mshukiwa mkuu, Joseph Irungu, Mugambi Laichena aliiambia mahakama watapinga ombi la upande wa mashitaka la kuzuia dhamana kwa mteja wao.

Jaji Wakiaga alimruhusu Joseph Irungu kwenda Hospitali ya Taifa Kenyatta kwa upasuaji chini ya usimamizi wa Gereza la GK Viwandani.

Wakati huo huo, mahakama imevionya vyombo vya habari kuripoti habari kwa hisia, ikisema vinaweza kuiharibu kesi hiyo.

“Mimi si jaji wa shule za kale na sipendi kushinikizwa kabla ya sijaisikia kesi. Vyombo vya habari vinapaswa kuwa makini na vinachoandika,” alionya Jaji Wakiaga.

Aidha aliuhoji upande wa mashitaka iwapo timu yake imekuwa ikivujisha taarifa nyeti kwa vyombo vya habari.

Hata hivyo, ulisema haufahamu kama kuna mtu miongoni mwao anayezungumza na vyombo vya habari.

Jaji Wakiaga alilamika kuwa baadhi ya ripoti za vyombo vinaharibu mwenendo wa kesi yao dhidi ya washukiwa hao wawili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles