NA WAANDISHI WETU – DAR ES SALAAM
MBUNGE wa Kilolo, Venance Mwamoto (CCM), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa kosa la kushindwa kumpeleka mahakamani mshtakiwa aliyemdhamini, Seth Mwamoto.
Mwamoto alimdhamini Seth ambaye ni kaka yake baada ya kufikishwa mahakamani hapo akidaiwa kujipatia fedha Sh milioni 28.8 kwa njia ya udanganyifu mali ya Perpetua Okololo na Robert Ndibalema mwaka 2011.
Inadaiwa mbunge huyo alikamatwa na polisi Agosti 30, mwaka huu na kuachiwa kwa dhamana Agosti 31 katika kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam na alifikishwa mahakamani jana.
Mahakama hiyo imemwamuru Mwamoto kulipa fedha hizo baada ya kudai kuwa kaka yake huyo hapatikani tangu alipomwekea dhamana.
Akizungumza mahakamani hapo, mmoja wa wadai, Perpetua, alidai kuwa Mwamoto alimtorosha mdaiwa wao baada ya kumwekea dhamana alipokuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi.
“Venance amemtorosha mdaiwa wetu (Seth) ambaye tayari alikamatwa na alikuwa anashikiliwa polisi ndipo naye akamwekea dhamana,” alisema Perpetua.
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.