MAKONDA ARUSHA VIJEMBE KWA WABAYA WAKE

0
1024

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


WAKATI baadhi ya watu wakionekana kumuombea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda afukuzwe, kiongozi huyo amewarushia vijembe wabaya wake hao.

Agosti 30, Rais Dk. John Magufuli, alimkemea Makonda kwa kitendo chake cha kutaka makontena 20 anayodai yana vifaa vya shule za Dar es Salaam, yatoke bandarini bila kulipiwa kodi ya Sh bilioni 1.2.

Baada ya kauli hiyo ya Rais, watu kwenye mitandao ya jamii walionekana kubashiri kuwa  siku za Makonda ofisini zinahesabika na kuwa wakati wowote Rais angetengua uteuzi wake.

Kutokana na hilo, Makonda aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa wahenga wana methali nyingine kama ‘mvumilivu hula mbivu’.

Akaandika tena: “Bado mnasubiri? Wahenga walisema subira yavuta kheri…maisha yanaendelea”.

Juzi, Profesa Mark Mwandosya naye aliandika katika ukurasa wake wa Twitter, akisema alivyofundishwa misingi ya utawala bora, mkuu wa nchi akimkosoa mtumishi hadharani, mtumishi huyo anapaswa kuandika barua ya kujiuzulu.

Ingawa hakumtaja Makonda moja moja, lakini ni wazi kuwa alimlenga mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa ni siku chache tu baada ya Rais Magufuli kumkosoa Makonda hadharani na kumtaka alipe kodi hiyo.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here