27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

KEITA ATETEA URAIS MALI

 

BAMAKO, MALI


RAIS Ibrahim Boubacar Keita, amechaguliwa tena kuendelea kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kushinda asilimia 67.17 ya kura katika uchaguzi wa marudio.

Waziri wa Serikali ya Mitaa wa Mali, Mohamed Ag Erlaf, alitangaza jana kuwa mpinzani wa Keita, waziri wa zamani wa fedha, Soumaila Cisse, alipata asilimia 32.83 ya kura katika uchaguzi huo uliofanyika Jumapili.

Cisse (68) pia aligombea urais dhidi ya Keita (73) wakati aliposhinda muhula wa kwanza mwaka 2013.

Hata hivyo, mwitikio wa wapigakura katika uchaguzi huo wa Jumapili ulikuwa chini baada ya kusimama katika asilimia 34.5.

Machafuko, msisimko mdogo miongoni mwa umma na tuhuma za udanganyifu zilitawala uchaguzi huo.

Jumatatu wiki hii, Cisse alisema atakataa matokeo yatakayotangazwa.

Keita ataapishwa Septemba 4 akiwa na matumaini ya kuimarisha mkataba wa amani wa mwaka 2015 baina ya Serikali, makundi yanayoiunga mkono na waasi wa zamani wa Tuareg.

Mali, taifa lisilo na bahari lenye makabila 20, ambako wakazi wengi wanashindia chini ya dola mbili kwa siku, liligeuka kuwa uwanja wa mapambano baina ya Serikali na makundi ya jihadi pamoja na machafuko kwa miaka kadhaa.

Mashambulizi ya makundi ya wanamgambo wajiitao wa Kiislamu, yamesambaa kutoka kaskazini hadi katikati na kusini mwa nchi na kuvuka mipaka ya mataifa jirani ya Burkina Faso na Niger.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles