27.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

KIZIMBANI KWA KUMWINGIZA MTOTO UUME MDOMONI, KUMLAWITI

Na waandishi wetu -DAR ES SALAAM


MKAZI wa Kimara Stop Over, Riziki Joseph (37), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya  Kinondoni, Dar es Salaam kwa shitaka la udhalilishaji wa kingono.

Akimsomea shitaka mbele ya Hakimu Anipha Mwingira, Mwendesha Mashtaka, Credo Rugaju, alidai Julai 24 mwaka huu maeneo ya Kimara Stop Over, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, mshtakiwa alimdhalilisha mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba (jina limehifadhiwa) kwa kumwingizia uume mdomoni na kisha kumlawiti.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo, na kuomba kupewa dhamana kutokana na hali yake ya kiafya aliyonayo.

Hata hivyo, Hakimu Mwingira alisema dhamana iko wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu mmojawapo awe mfanyakazi kutoka taasisi inayotambulika na Serikali pamoja na bondi ya Sh 500,000.

Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana na kesi yake itatajwa tena Septemba 3, mwaka huu.

Habari hii imeandaliwa na ZAKIA NDULUTE (UoI), EMMY LEONARD (DACICO), STELLA SADOCK (DSJ) Na ERICK MUGISHA (DSJ)

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Ingefaa serikali iwe na fungu la kupima DNA ili wahalifu kama wabakaji wapatikane kwa vidhibiti kwani amemuingiza mdomoni na kumlawithi-Chembe zake zingedhihirishwa na dhamana isingetolewa. DNA idhihirishwe kabla ya kutoa dhamana huenda mbakaji alitumia kodomu lakini alimgusa kwa mikono pia. Iwe tabu kudhihirisha kwa DNA mpaka apewe dhamana?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles